JIFUNZE KIARABU

Jifunze leo Kiarabu ,Usisumbuke tena ni wapi utajifunza kiarabu ,hakikisha unatembelea Website hii usipitwe na mafunzo mbalimbali.




تعلم اللغة العربية 

JIFUNZE LUGHA YA KIARABU

Lugha ni moja ya nyenzo za mawasiliano kati ya mtu mmoja na mwengine, hivyo kujifunza lugha ngeni ni muhimu mno hasa kwa maisha ya sasa,  unaweza kupoteza fursa nyeti za kimaisha sababu kutokujua lugha ya watu.

Binafsi nipo kwenye biashara na waarabu sio sababu kwamba Mimi ni mtaalamu wa biashara lahasha, bali wamenichukua kwa sababu naweza kufahamiana nao lugha moja na tukaelewana. Ukiongezea uaminifu na nk.

Umuhimu wa kujifunza lugha hauishii tu kwenye fursa za ajira bali hata kujiokoa wewe mwenyewe na majanga au changamoto ambazo zisingekupata kama ungekua unaijua lugha.

Mfano: umenunua dawa ambayo hutakiwi kutumia zaidi ya mara moja ww ukatumia mara mbili au zaidi. Pia unawezakua umepita sehemu hatarishi ambayo haitakikani kupita  kwa kutokujua kusoma tangazo la "Tahadhari usipite hapa''  yakakukuta mbaya.

Umuhimu wa kujifunza lugha ngeni ni mkubwa mno siwezi kumaliza kila kitu tosheka na hilo.

Kwenye Blog yako pendwa ya Sulomy academy utajifunza mengi kuhusu lugha ya Kiarabu.

Karibuni na Asanteni.

tembelea Channel yetu kujifunza zaidi kuhusu lugha ya Kiarabu