JIFUNZE KOZI FUPI YA UGONJWA WA BAWASIRI

Sehemu ya 01

Kozi fupi zinazohisi afya yako utazipata hapa katika blogg yako pendwa, na kupitia Whatsapp group 

Jiunge na group la WhatsApp

Jiunge na channel ya WhatsApp


Tuanze na kozi yetu sehemu ya kwanza 01



SULOMY HEMOROID COURSE

Siku ya 1: Utangulizi wa Bawasiri

Karibu kwenye kozi ya kitaalamu ya Sulomy kuhusu ugonjwa wa bawasiri.

Leo tutajifunza mambo ya msingi kuhusu ugonjwa huu.

1. Bawasiri ni nini?

Bawasiri ni hali ya uvimbe au kuvimba kwa mishipa ya damu katika sehemu ya mwisho ya njia ya haja kubwa (rectum) au kwenye tundu la haja kubwa (anus).

Ugonjwa huu husababisha maumivu, muwasho, kutokwa damu au nyama kutoka wakati wa choo.


2. Aina za Bawasiri:

Bawasiri ya ndani: Hii hutokea ndani ya njia ya haja kubwa. Mara nyingi haitoi maumivu sana, lakini huweza kuvuja damu.


Bawasiri ya nje: Hutokea nje ya tundu la haja kubwa. Huambatana na maumivu makali na kuwashwa.


3. Dalili kuu za bawasiri:

- Kutokwa damu wakati wa kujisaidia

- Kuwashwa au maumivu sehemu ya haja kubwa

- Kujisikia kama kuna kitu kimebaki au kuvimba

- Kutoka kwa nyama au uvimbe wakati wa choo


4. Sababu kuu zinazosababisha bawasiri:

- Kukosa ulaji wa vyakula vyenye nyuzinyuzi (fiber)

- Kukosa maji ya kutosha

- Kukaa muda mrefu chooni au kushinikiza sana

- Mimba kwa wanawake

- Kunyanyua vitu vizito

- Uzito mkubwa wa mwili


Ushauri

Ongea na mtaalamu wa afya

Bawasiri inaweza kudhibitiwa na kutibika kwa kutumia njia za asili ikiwa itagundulika mapema na kufuatwa maelekezo sahihi.

“Ukiona dalili hizi, usikae kimya – suluhisho lipo kwa njia asilia!”

Mawasiliano 

+255 718 958 410 / +255 626 908 654

Endelea na sehemu ya pili