KOZI FUPI YA KUJIFUNZA UGONJWA WA VIDONDA VYA TUMBO NA MATIBABU YAKE

 SEHEMU YA 5: 

Chanzo Kikuu cha Vidonda vya Tumbo (H. pylori na Tindikali)

Salaam mpenzi mshiriki,

Leo tutaangazia chanzo kikuu cha vidonda vya tumbo ambacho watu wengi hawakijui kwa undani. Hii ni hatua muhimu ya kuelewa tatizo kabla ya kuingia kwenye tiba ya kina.


1. H. pylori – Bakteria wa Siri



Huyu ni bakteria anaepatikana tumboni kwa watu wengi.

Huishi kwa miaka bila dalili, lakini akipoa kinga ya mwili, huanza kushambulia ukuta wa tumbo.

Hutoa sumu inayochimba ukuta wa tumbo hadi kuleta vidonda.

Anaweza pia kusababisha saratani ya tumbo kwa baadhi ya watu.

Jiunge na channel ya WhatsApp

Dalili za H. pylori:

- Maumivu makali au kuchoma tumboni

- Kuvimba tumbo

- Kikohozi kisichoisha (kwa baadhi ya watu)

- Harufu mbaya mdomoni

- Kukosa hamu ya kula


2. Tindikali Kupita Kiasi (Acid Overproduction)

Tumbo hutoa tindikali kusaidia usagaji chakula.

Lakini kuna wakati uzalishaji unazidi na kuharibu ukuta wa tumbo.

Hali hii inachochewa na:

- Msongo wa mawazo

- Ulaji holela wa vyakula vyenye asidi kali

- Kutokula kwa muda mrefu

- Kunywa kahawa au chai kali kupita kiasi


3. Jinsi ya Kudhibiti Hali Hizi Kwa Tiba Asilia

- Mimea kama tangawizi, mlonge, bizari, na ganda la chungwa huzuia bakteria ya H. pylori.

- Iliki, mrehani, karafuu na papai husaidia kuponya na kulinda ukuta wa tumbo.

- Kunywa maji ya uvuguvugu kabla ya chakula huondoa tindikali kali tumboni.


Ujumbe wa Leo:

> “Tiba ya kweli huanza kwa kujua chanzo. Usiponyeshe tu maumivu – ponyesha mzizi wa tatizo.”

Mawasiliano na Dr, Sulomy. 

0626908654/0718958410

Kupata masomo yalokupita 

Sehemu ya 01

Sehemu ya 02

Sehemu ya 03

Sehemu ya 04